Saturday, June 22, 2013

On 8:16 AM by Shambani Solutions   No comments


D’Salaam.Wakulima wa zao la muhogo nchini,watanufaika na fursa mpya za kibiashara zinazoendelea kujitokeza iwapo watazingatia viwango vilivyowekwa na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akizungumza katika mafunzo ya siku moja ya wakulima wa zao la muhogo,Mtaalamu wa Ongezeko la Thamani katika Mazao kutoka Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kitropiki(IITA),Abbas Adebayo amesema ni muhimu kwa wakulima kuzingatia viwango vilivyowekwa ili waweze kujikwamua katika umaskini kutokana na zao hilo.

“Kama wakulima watafuata viwango vilivyowekwa katika kulima na kutayarisha muhogo vizuri, wanaweza kuuza nje ya nchi ambako ongezeko la mahitaji linakuwa kila kukicha,” anasema Abbas.
Alisema nchi zenye viwanda zinahitaji wanga wa muhogo katika kujiendesha na zimekuwa zikununua kutoka Nigeria,Ghana,Venezuela na kwingineko kitu ambacho Watanzania wanaweza kukifanya kama watafuta maelekezo ya wataalamu

0 comments:

Post a Comment