Wednesday, June 19, 2013

On 2:48 AM by Shambani Solutions   No comments


Muleba. Wakulima wa zao la kahawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Kagera, wametakiwa kuacha tabia ya kuvuna zao hilo likiwa bichi ili kuweza kupata soko katika vyama vya ushirika.

Ofisa Kilimo Muleba, Justinian Muchunguzi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili kuhusiana na msimu wa mavuno ya kahawa wilayani humo ambao umeanza tangu Mei mwaka huu.

Muchunguzi alisema baadhi ya wakulima wanavuna kahawa mbichi na kuianika chini ya udongo na inapopelekwa sokoni haikutwi na ubora, hatimaye mkulima kupata fedha kidogo katika mauzo yake.

Aidha, aliwataka mabwana na bibi shamba katika halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha wanawaelimisha wakulima kuhusu uanikaji wa kahawa kwa kutumia chanja ama magudulia, ili kupunguza kuuza mazao yao yasiyokuwa na tija katika soko la dunia.

Uchumguzi uliofanywa na gazeti hili wilayani humo katika Kata za Kagoma, Kishanda na maeneo ya visiwani umebaini kuwa bado wananchi wanavuna zao hilo likiwa bichi na kuanika chini ya mchanga bila hatua zozote kuchukuliwa na viongozi wa maeneo hayo


0 comments:

Post a Comment