Wednesday, June 19, 2013

On 2:43 AM by Shambani Solutions   No comments


Mbulu. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara,wametakiwa kusimamia utekelezaji wa shughuli za ufufuaji na uendeshaji wa majosho katika kata zao,ili kuboresha hali ya mifugo na hatimaye kuongeza pato la wafugaji na Taifa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu,Fortunatus Fwema aliyasema hayo alipokua akifungua mafunzo ya siku tano ya ufufuaji wa majosho,yaliyofadhiliwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la SNV. Fwema alisema kufanya hivyo kutawasaidia katika kupunguza idadi ya vifo vya mifugo vinavyotokana na magonjwa ya kupe,kwani vifo vingi vya mifugo hasa ng’ombe husababishwa na mifugo kutoogeshwa na dawa

0 comments:

Post a Comment