Monday, June 17, 2013
On 4:00 AM by Shambani Solutions No comments
Dar es Salaam.Wakulima wadogo Kusini mwa Sahara Afrika, Afrika ya Kati na
Asia huenda wakaanza kunufaika baada ya Benki ya Dunia kupitia Taasisi yake ya
Fedha (IFC) kuingia mkataba na Umoja wa Wafanyabiashara za Nje (ETG) unaolenga
kuwawezesha wakulima hao. Mkurugenzi wa IFC, Uzalishaji , Biashara ya Mazao ya
Kilimo na Huduma, Oscar Chemerinsiki alisema wamefikia hatua hiyo baada ya
kufanya utafiti, wanaamini kwamba itawasaidia wakulima wadogo kufikia malengo
yao ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kuwa na soko la uhakika la mazao yao.
Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba IFC inaendelea na uhusiano katika kuwekeza, ambapo imeanza kushirikiana kwa kuwapamkopo ETG tangu mwaka 2010 na kwa imejipanga kuwekeza dola biloni 4 kwa biashara ya mazao., Naye Mwenyekiti wa ETG, Ketan Patel alisema kwa kutumia miundombinu ya usindikaji na kuhifadhi itatoa vyanzo bora vya vyakula, hivyo kuuzalisha fursa za ajira
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment