Sunday, June 30, 2013
On 6:47 AM by Shambani Solutions No comments
Rais wa Uganga Mh Yoweri Museveni |
Rais Museveni ambaye alikuwa akizungumza katika
Kongamano la Kimataifa linalohusu majadiliano ya wazi kwa manufaa ya
wote (smart partnership dialogue) alisema nchi nyingi za Afrika bado
zinaendelea kuhubiri maendeleo yatokanayo ya sekta ya kilimo ilhali
zikifahamika wazi kuhusiana na tatizo la ardhi.
Alisema utashi wake unamtuma kuamini kuwa iko siku
bara la Afrika litajikuta katika hali ya kukosa mwelekeo kutokana na
uhaba wa ardhi ambao alisema umeanza kujitokeza katika maeneo mengi.
Akitetea hoja yake hiyo, Museveni alitolea mfano
hali ilivyo nchini Kenya ambako alisema kuwa moja ya tatizo kubwa
linalojitokeza sasa ni kuhusiana na umiliki wa ardhi ambako idadi kubwa
ya watu wanaendelea kulalamika kutokana na ardhi hiyo kuhodhiwa na
wachache.
Pamoja na kutoa angalizo hilo, Rais Museveni
alizishauri nchi za Afrika kuanza kufikiria njia nyingine za kujiletea
maendeleo ikiwamo pia kuanzisha mikakati ya kuwa na viwanda vya kutosha.
kwani bila kufanya hivyo dhana ya kuwa na maendeleo endelevu huenda
isifikiwe kwa wakati.“Lakini pia napenda niwasihi Waafrika wenzangu
tunapaswa kutambua kuwa kuendelea kutegemea rasilimali pekee
hakutatusaidia,” alisema
Kongamano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya
kwanza barani Afrika, ni jukwaa linalowakutanisha viongozi wa
kiserikali, wanasiasa pamoja na wataalamu kwa ajili ya kuwa na
majadiliano ya pamoja ambayo yanazingatia fursa sawa kwa pande zote.
Viongozi wanahudhuria kongamano
hilo ambalo linaendeshwa na Rais Jakaya Kikwete na wanatazamiwa
kuendelea na majadiliano yatakayogusia maeneo ya ubora na viwango vya
ufanyaji biashara, mahitaji yanayopaswa kuzingatiwa ili kuleta mageuzi
kwa maisha ya wanawake kwenye sekta ya teknolojia na uendelezwaji wa
rasilimali.
Wakati akifungua majadiliano hayo, Rais Jakaya
Kikwete alizitaka nchi za Afrika kubadilika kwa kuendeleza wasomi, ili
wawe chachu ya kubuni na kuibua vyanzo vya maendeleo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment