Sunday, June 30, 2013
On 8:42 AM by Shambani Solutions 1 comment
Wakati vijana wengi tumekuwa tukilalamikia juu ya
tatizo la kutokuwepo kwa ajira hali inayosababisha umaskini mkubwa miongoni mwa
vijana wengi, huku kumekuwa na ongezeko la vijana wengi wanaohama vijijini na kuhamia
mijini kwenda kutafuta unafuu wa maisha hali inayowafanya vijana wengi kuishi
katika mazingira magumu wawapo mijini kutokana na ukweli kwamba wengi wao
hawana ujuzi wa kuwawezesha kuishi mijini kwani sehemu kubwa ya shughuli za
mjini zinaitaji mtu awe na ujuzi Fulani ili afanikiwe.
Masanja katika harakati za kilimo |
Hali imekuwa tofauti kwa Msanii na mchekeshaji
maarufu wa kipindi cha Ze Orijino Comedy,
Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ambaye amesema kuwa vijana
wanapaswa kufikiria namna ya kuwekeza vijijini hasa kwenye mashamba kwani huko
kuna fursa nyingi zenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha ya vijana
walio wengi ambao wameng’ang’ania mjini na kuendekeza majivuno yasiyo na msingi
huko mijini huku maisha yao yakiendelea kudorora siku hadi siku
Akizungumza na mwandishi wetu Masanja
Mkandamizaji alisema anafurahi kwani mwaka huu amefanikiwa kuvuna tani kadhaa
za zao la mpunga katika shamba lake lililopo Mbarali Estate.
“Nimelimia Mbarali Estate namshkuru Mungu kwa
kufanikiwa kuvuna mpunga wangu baada ya kuwekeza shamba lenye ukubwa wa ekari
15, huu ni uwekezaji mzuri unaotoa matunda kwa muda mfupi iwapo utahudumia
shamba lako ipasavyo.”
“Vijana wengi wana nguvu na uwezo wa kuingia
mashambani ila wanaendekeza ‘usharobaro’ kitu ambacho hakina mavuno kwao,”
alisema Masanja aliyetumia mashine ya kisasa katika zoezi hilo.
Aliwaasa vijana kutokukimbia mashambani na badala
yake wajiunganishe katika vikundi vya kujikwamua kiuchumi hali itakayowawezesha
vijana kupata elimu na uwezo wa kulima kisasa ili wapate mazao mengi nay a kutosha
hali itakayowapunguzia vijana walio wengi ugmumu wa maisha.
Masanja ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya New
Jerusalem alisema: “Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya
uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Ze Komedy, kupitia hilo nina
washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu,
naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti,” alisisitiza!
Kwa sasa, Masanja anahudhuria ibada katika kanisa
la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari
album yake ya ‘Hakuna Jipya’ iko mitaani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
All I can say to Masanja, It's big up for trying to overcome the challenges other faces but for him he choose to try different way of self employed which has been a good example to the people, if everyone can think and consider that employment is not based on Government but trying to your best and manage whatever you can you may come out of poverty.
ReplyDeleteBig Up Mr E... M, Masanja