Sunday, February 24, 2013
On 2:41 AM by Shambani Solutions No comments
NDG PHILEMON LUHANJO - KATIBU MKUU KIONGOZI ALIYESTAAFU |
Nimeitumikia serikali
katika nyadhifa mbalimbali kwa muda wa miaka 35 tangu mwa 1977 hadi mwa 2011 nilipostaafu kipindi hicho
chote nilikuwa nafanya kazi za ofisini lakini nilipenda sana siku ntakapostaafu
nifanye kazi za tofauti na kazi za makaratisi, na sasa baada ya kustaafu nimeamua kujishughulisha na kilimo kama shughuli yangu rasmi.
Napenda sana kilimo na
mimi ni mmoja wa watu walioanzisha kauli mbiu ya KILIMO KWANZA nilipokuwa
katika baraza la taifa la biashara kama mwenyekiti wa kamati ya utendaji,
tulianzisha kauli mbiu hiyo kwa kuwa kila jambo linategemea kilimo na pia
kilimo ndo uti wa mgongo wa taifa letu na kinaajiri asilimia 80 ya watanzania
wote. Maneno hayo yalisemwa na aliyekuwa katibu mkuu kiongozi ndg Philemon
Luhanjo akiwa katika mshamba yake ya chai mkoani njombe
Akizungumzia namna
anayotumia mda wake mwingi kwa sasa kujishughulisha na kilimo anasema tangu
aingie shambani mwaka jana amekuwa shambani hadi leo (February 20 2013) baada
ya hapo ntarudi dsm kidogo kwa likizo kisha ntarudi tena shambani kuhudumia
mashamba yangu
Luhanjo aliendelea
kusema, ameamua kujishughulisha na kilimo kwa kuwa anakifahamu vizuri na kupitia
makala hii anapenda kuhamasisha watumishi mbalimbali walio maofisini
kutokipuuza kilimo badala yake wageukie kilimo maana kina faida kubwa sana
Aliendelea kutoa
motisha chanya kwa wastaafu wengine wamtembelee ili wajifunze kutoka kwake
maana wastaafu wengi hukimbilia kufanya biashara zinaoweza kuwalipa kwa muda
mfupi na kukiacha kilimo kwa kuhofia uhaba wa mvua na sababu zingine mbalimbali
ikiwemo kukitazama kilimo kama shughuli wa watu waliopoteza matumaini, wasio na
elimu na waliokosa shughuli zingine za kufanya
Luhanjo alieanza kujishughulisha
na kilimo mwaka 2010 kabla ya kustaafu hakusita pia kueleza changamoto
mbalimbali alizokutana nazo mpaka sasa kama vile uhaba wa mvua, wadudu
waharibifu, soko kutokuwa la kuaminika hasa pale wakulima wanapozalisha kwa
wingi sana bei za mazao hushuka na kupunguza faida kwa mkulima
Pia aliishauri serikali
kuanzisha utaratibu wa maafisa kilimo kusomea zao moja ili ajikite kisawasawa
katika kulifahamu zao hilo hatimaye afisa huyu wa kilimo aweze kuwasidia
wakulima kwa ufanisi
Fuatilia habari hii kwa kina
kupitia: http://www.habarileo.co.tz/index.php/nyota/9220-philemon-luhanjo-ktaibu-mkuu-kiongozi-aliyegeuka-mkulima
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment