Tuesday, February 26, 2013
On 1:00 PM by Shambani Solutions No comments
Vijana wa JKT wakiwajibika kibaha |
Kufufuliwa
kwa hayo mashamba hilo kumeelezwa kuwa kutarahisisha upatikanaji wa chakula kwa
askari waishio katika kambi hiyo pamoja na wale watakaokuwa wanapita kwa ajili
ya kupata mafunzo ya kijeshi.
Hayo
yamebainishwa hivi karibuni kwenye mahafali ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya
jeshi hilo yaliyopewa jina la Operation Sensa 2012-2013 yaliyofanyika kwenye
viwanja vya mabatini Kibaha wakati wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi.
Walisema
kutokana na mafunzo waliyoyapata kwa kipindi cha miezi sita wakiwa kambini hapo
pamoja na mambo mengine,wameweza kupata uelewa wa namna ya kuendesha kilimo cha
kisasa,ujasiriamali,uzalendo pamoja na upendo na ushirikiano katika kufanya
kazi.
Aidha
walisema kuwa mafunzo waliyoyapata yatakuwa kichocheo kikubwa kwao mahali
popote watakakokwenda na kuahidi kuwa watakuwa tayari kuitumikia nchi yao na
kuhakikisha kudumisha amani iliyopo.
Kwa
upande wake, Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Brigedia Jenerali Mwanamakala
Kilo ambaye ni Mkurugenzi kutoka Suma Jkt,aliwataka vijana hao kutojihusisha na
tamaduni za kigeni ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwaharibu vijana wengi
kitabia na badala yake wajijengee staha katika uvaaji wa mavazi na vitendo
vinavyokubalika na jamii.
Alisema
kuwa hivi sasa vijana wengi wamejiingiza kwenye tamaduni za kigeni kwa kufanya
vitendo visivyokubalika na jamii ya Mtanzania na kwamba hali hiyo ni lazima
ipigwe vita kwa nguvu katika maeneo yote.
“Utamaduni
wa kigeni ambao hauleti sura nzuri ni sawa na bidhaa bandia isiyokubalika hapa
nchini,nawaomba huko muendako ili muendelee kuwa vijana wanaokubalika ni vema
mkajiepusha na kujiingiza katika kundi hilo”Alisema
Kambi
ya Ruvu JKT ni miongoni mwa kambi za jeshi kongwe ambazo zinazalisha vijana
wengi kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi na kwamba katika mahafali hayo vijana
wapatao 989 kati yao wavulana 754 na wasichana 240 wakiwa na viwango vya elimu
mbalimbali walihitimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment