Sunday, May 31, 2015

On 1:14 AM by Shambani Solutions   No comments

Kampuni ya mawasiliano ya Vodafone imezindua mpango maalumu wa kuboresha maisha ya wakulima wadogo wa Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa Tanzania.Nchi zingine zitakazotekeleza mpango huu ni Kenya,Ghana na India.

Mpango wa Vodafone Kilimo Klub unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo kwa kuwaongezea uzalishaji kupitia kisaidizi maalumu ambacho ni simu za mkononi.Mpango huu kwa mara kwa kwanza ulizinduliwa nchini Uturuki mwaka 2009.Asilimia 25 ya wakazi wa nchi hiyo ni wakulima na kupitia mpango huu zaidi ya wakulima milioni 1.2 wamenufaika kwa uzalishaji wa mazao kuongeka ambako kunaendana sambamba na ongezeko la kipato chao.

Kilimo Klub itatekelezwa kwenye nchi husika kulingana na mahitaji ya wakulima yaliyopo kwenye nchi hizo ila italenga kutumia simu za mkononi kuwarahishia wakulima wadogo maisha kwa kuwapatia taarifa za masoko,hali ya hewa,na huduma za kifedha.Mpango huu pia utatekeezwa katika nchi ya New Zealand ambayo licha ya kwamba imepiga hatua kubwa katika sekta ya kilimo lakini utalenga zaidi kuwakomboa wakulima wadogo nchini humo kuongeza uzalishaji.

Mtendaji Mkuu wa Vodafone anayesimamia kanda za Afrika,Mashariki ya Kati na Asia Serpil Timuray amesema : “Moja ya tatu ya watu duniani wanategemea kupata chakula kilichozalishwa na wakulima wadogowadogo wenye vipande vidogo vya ardhi visivyozidi hekari 2.Teknolojia ya simu za mkononi ikutumika ipasavyo inaweza kubadilisha maisha ya wakulima hawa yakawa bora kutokana na ongezeko la uzalishaji utakaowezesha pato lao kuongezeka.Kilichotokea nchini Uturuki kupitia teknolojia ya simu za mkononi kubadilisha maisha ya wakulima ni ushahidi tosha kuwa Kilimo Klub ni ukombozi kwa wakulima.

Serpil Timuray aliongeza kusema: “Kwa kadri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka kuna haja ya kuangalia jinsi ya kuongeza uzalishaji wa chakula kwa kuzingatia njia bora za matumizi ya ardhi.Mpango kama Kilimo Klub wa Vodafone ni mzuri na una msaada mkubwa kuboresha maisha ya wakulima na kuhakikisha kunakuwepo na chakula cha kutosha.

Uzinduzi wa mpango wa Kilimo Klub wa Vodafone kwenye nchi 4 leo umekwenda sambamba na uzinduzi wa sinema inayoonyesha huduma sita zilizopo chini ya mpango huu zilivyoweza kuboresha kipato cha wakulima 70 milioni nchini India kwa kuwawezesha kujipatia kipato cha dola za Kimarekani bilioni 9 kwa mwaka.Familia nyingi za wakulima wa India zinaishi kwa wastani wa matumizi yasiyozidi dola 4 za Kimarekani kwa siku.

Kwa mujibu wa ripoti ya Connect Farming ya India iliyochapishwa na Vodafone imeonyesha jinsi wakulima wengi walivyonufaika kupitia huduma zipatazo 6 zinazotolewa kwao kupitia simu zao za mkononi na kufanikisha kipato cha wakulima 70 milioni nchini India kwa kuwawezesha kujipatia kipato cha dola za Kimarekani bilioni 9 kwa mwaka.

Ripoti hiyo iliyofanywa na taasisi ya Accenture Strategy kwa ufadhili wa Vodafone Foundation imebainisha kuwa matumizi ya simu kurahisisha kilimo kumewezesha wakulima nchini India mapato yao kupanda kufikia wastani wa dola Marekani 128 kwa mwaka kwa zaidi ya nusu ya wakulima nchini humo tofauti na pato la dola ambapo hata hivyo bado kuna wakulima wengi wanaoishi kwa chini ya dola 4 kwa siku wakiwa wanakabiliwa na changamoto ya kupata chakula cha kutosha na kusomesha watoto.

Kwenye ripoti hiyo imebainishwa kuwa nchi ya India ni moja ya nchi inayozalisha chakula kwa wingi duniani ikiwa na wakulima wapatao milioni 200 na karibu nusu yao wakifanya kazi kama vibarua kwenye mashamba na asilimia 62 ya wakulima nchini humo wakiwa wanamilik mashamba madogo yasiyofikia hekari 1 huku wakiwa wanakabiliwa na changamoto za kupata taarifa za masoko,mbinu bora za kilimo cha kisasa na taarifa zinginezo kama vile hali ya hewa.

Vodafone na Accenture Strategy zimebuni nyenzo sita za kubadilisha maisha ya wakulima nchini India kuwa murua kupitia simu za mkononi ambazo ni kutoa huduma zifuatazo:

Kutoa taarifa za kilimo-Huduma hii inatoa taarifa za hali ya hewa,matukio mbalimbali kama vile ni msimu gani wa kupanda mazao na kuvuna.Huduma hii itawaongezea karibu wakulima milioni 60 nchini India kipato cha wastani wa Dola za Kimarekani 89 ifikapo mwaka 2020.

Kutoa risti-Huduma hii inawawezesha wakulima kupunguziwa adha ya kupunjwa wanapouza mazao yao na pembejeo za kilimo kwa kuwa inadumisha uwazi katika masuala ya malipo na kuondoa udanganyifu.

Kufanya malipo na kupata mikopo-Kuwawezesha wakulima kutafuta huduma mbalimbali za kuwarahishia kazi yao na kufanya malipo kutumia simu zao kama vile huduma ya Vodafone ya M-Pesa,ilizinduliwa nchini India mwaka 2013 na kwa muda mfupi imeonyesha mafanikio makubwa ya kufanya malipo na hadi kufikia mwaka 2020 itakuwa imewanufaisha wakulima kwa kiasi cha Dola za Kimarekani 690 kwa mwaka ambapo itawaongezea wakulima wastani wa asilimia 39 mapato.

Ukaguzi na utunzaji nyaraka za kumbukumbu-Mpango huu unawezesha wakaguzi kupitia kumbukumbu za wakulima kupitia njia ya kieletronikali kupitia data za simu na inasaidia kuboresha ufanisi wa kazi za wakulima na umeweza kuwaongezea baadhi ya wakulima pato kufikia dola za Kimarekani 612.

Kujenga mtandao bora wa uuzaji mazao- Mpago huu unawezesha wakulima unawawezesha wakulima kuuza mazao yao kwenye vyama vya ushirika kwenye maeneo na kubadilishana taarfa na kulipwa kutma njia ya simu. Njia hii itawezesha hadi kufikia mwaka 2020 itaweza kuongeza pato la wakulima kufikia dola za Kimarekani 271 na imeongeza mapato ya wakulima wengi kwa asilimia 50 kwa sasa.

Kuwezesha upatikanaji wa simu zinazotumia internet (Smartphone)-Simu hizi ni rahisi kuwezesha wakulima kupata taarifa japokuwaa bao ni za gharama kubwa kwa wakulima wengi vijijini kumudu kuzinunua ingawa kadri ya siku zinavyosonga mbele zinazidi kushuka bei.Hadi kufikia mwaka 2020 simu hizi zikitumiwa ipasavyo zaidi ya wakulima milioni 4 pato lao litaongezeka hai kikia Dola za Kimarekani 675.

0 comments:

Post a Comment