Tuesday, August 6, 2013

On 5:24 AM by Shambani Solutions   No comments


Lushoto. Wakulima wa Njegere Wilaya ya Lushoto,  mkoani Tanga, wameomba Serikali kuwatengenezea miundombinu ya umwagiliaji maji kwenye mashamba yao na kupunguza bei za pembejeo, ili kutekeleza Sera ya Kilimo Kwanza.

Akizungumza kwenye  shamba darasa juzi, Sadat Amir alitaka  Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika  kuwajengea mfumo wa maji ambao utawezesha kuendesha kilimo chao hasa baada ya mabadiliko ya tabianchi.

Naye Meneja wa Shirika la Oxfam Wilaya ya Lushoto,  Eustard Rwegoshora, alisema wakulima wengi wamekuwa wakipata changamoto nyingi kwa kilimo hicho kwa kutozingatia elimu ya wataalamu.
Alisema wamekuwa wakiwafuata wakulima shambani kuwapa elimu, jinsi ya kupata mazao kwa wingi ila wengi wanashindwa kufuata maelekezo ya wataalamu.

0 comments:

Post a Comment