Wednesday, July 31, 2013

On 3:00 PM by Shambani Solutions   No comments

Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) limeanza kutoa mafunzo elekezi kwa wasindikaji wa mafuta ya alizeti pamoja na wakulima wa zao la alizeti lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa usindikaji wa mafuta hayo.

Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku mbili, Mshauri wa Masuala ya Maendeleo ya Kilimo Mnyororo na Uthaminishaji wa Mazao, Anastazia Kondowe alisema mafunzo hayo yatawafanya wasindikaji pamoja na wakulima kuwa tayari katika kuifanya sekta hiyo kuwa ni yenye tija.

Alisema mafunzo yatawafanya wasindikaji mkoani hapa kuwa na umoja utakaotambulika kisheria na hivyo kupata mitaji ya mikopo kutoka kwa wadau mbalimbali.

Alisema mradi huo unaoendeshwa na SNV utatoa elimu kwa wakulima 550 wilaya za Mvomero na Ulanga kwa kuwashirikisha maofisa ugani ili kufahamu mbegu bora za alizeti, matumizi sahihi ya pembejeo.

0 comments:

Post a Comment