Wednesday, July 31, 2013
On 2:33 PM by Shambani Solutions No comments
Mwenyekiti wa Jukwaaa la Katiba - ndugu Deus Kibamba |
Mchakato
wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi haujamzungumzia
mkulima na nafasi yake katika kuleta maendeleo. Maneno hayo yamesemwa na Deus
Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania alipokuwa anaongea na wanachama
wa Muungano Wa Vikundi vya Wakulima Tanznia(MVIWATA) walipokuwa katika mjadala
wa katiba mpya na nafasi ya mkulima katika katiba mpya
Vilevile Kibamba anasema kama ambavyo mkulima amekuwa akipuuuzwa kwa namna
mbalimbali, hata Rasimu ya Katiba inayojadiliwa haijaeleza kinaga ubaga nafasi
ya mkulima na ushirki wake mzima katika kumiliki uchumi wa nchi
“Tanzania ni nchi ya Wakulima na Wafanyakazi rasimu ya katiba mpya haielezi
nchi hii ni ya akina nani, pamoja na kutoeleza, mimi nadhani nchi hii kwa sasa
ni ya wafanyabiashara na wawekezaji,” anasema Kibamba. Aliendelea kubainisha kuwa mawazo ya wakulima hao ni muhimu ili haki zao
ziweze kuingizwa, badala ya sasa ambazo ‘zimechomekwa’ katika makundi madogo
wakati wenyewe ndio kundi kubwa.
Kwa mujibu wa Kibamba, wakulima hao wapiganie ardhi, rasilimali na misitu
ambayo ni mambo muhimu kwa wakulima, ili yaweze kuingizwa katika rasimu, badala
ya kuishia kuyaona kama mambo ambayo si ya Muungano.
Pamoja na kuikosoa rasimu hiyo, Kibamba anasema walau imeonyesha kuwa
inaandaliwa kwa kuwashirikisha wananchi, wakiwamo wakulima na wafanyakazi, na
maandalizi yake yanafuata utaratibu wa kisheria, hivyo Katiba itakayopatikana
itakuwa halali ukilinganisha na katiba za mwaka 1961, 1962, 1964, 1965 na hii
ya sasa ya 1977 kwani hizi katiba ziliundwa na watu wachche na wananchi
walitakiwa wajifunze katiba mara baaada ya kupitishwa” aliendelea kusema.
Source; http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Kibamba--Rasimu-ya-Katiba-mpya-haimtaji-mkulima/-/1597592/1932746/-/pjxf82/-/index.html
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment