Saturday, June 8, 2013

On 4:32 AM by Shambani Solutions   No comments
Tumetoka Mbali; Mwenyekiti Wenu Kwenye Shamba Lake La Viazi 1991!
Pichani ni kijijini Igagala, 1991. Ndio kwanza nimetoka kwenye Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT)- Operesheni Kambarage. Na nimekondeana pia, lakini , ni mwenye nguvu za kulima!

Naam, kwa hiyari yangu, na kwa vile sikupata kuishi maisha ya kijijini kwa muda mrefu, nikaamua kuishi maisha ya kijijini kwa mwaka mmoja na nusu. Niliishi kijijini Igagala wilayani Njombe, mbali kabisa na Dar es Salaam nilikozaliwa na kukulia. Nilitaka kuishi na kujifunza maisha ya kijijini. Ndio, nilitaka kuyafahamu kwa karibu maisha ya wanavijiji wa nchi hii. Kuwaelewa wanavijiji wanavyofikiri.

Hivyo, miongoni mwao nami nilikuwa mkulima kijana wa zao la viazi. Wakati huo, mbolea ya kupandia aina ya ’ DAP’ tulinunua kwa shilingi elfu tano kwa mfuko mmoja wa kilo 50. Ulitosha ekari moja. Bei ya sasa ni zaidi ya shilingi themanini elfu. Mbolea ya Urea na ’ CAN’ enzi hizo tulinunua kwa shilingi elfu nne. Sasa inauzwa kwa zaidi ya shilingi sabini elfu. Gharama zote hizo bado hujaongeza gharama za kuifikisha mbolea shambani.

Naam, tumetoka mbali.

Picha kwa hisani ya Mjengwablog,
Iringa.

0 comments:

Post a Comment