Monday, March 25, 2013

On 12:40 PM by Shambani Solutions   No comments

Zaidi ya matrekta 66 yaliyotolewa kama mkopo kwa baadhi ya wakulima na Mbunge wa Hanang’, Dk Mary Nagu yanadaiwa kuchangia kuongezeka kwa uzalishaji mazao ya chakula na biashara.
Katibu wa mbunge huyo, Mathew Darema alisema matrekta hayo yameleta mageuzi makubwa kwenye kilimo cha biashara na chakula kwa wakulima wa wilaya hiyo. Darema alisema Dk Nagu ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), alifanikisha mkopo wa matrekta hayo yaliyotolewa na Shirika la Uchumi na Maendeleo la JKT (Suma JKT) kupitia Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB).
Alisema matrekta hayo yameleta ufanisi wa kilimo hivi sasa, kwani mazao mbalimbali ya biashara na chakula ikiwamo alizeti, mahindi, maharagwe na mtama mweupe yameongezeka kwa kiwango kikubwa.
Matrekta haya yamechangia kushusha bei ya kulima, kwani awali ilimbidi mkulima kuwa na Sh60,000 au zaidi ili kulima shamba, hivi sasa hata ukiwa na Sh40,000 unalima shamba lako alisema Darema.
Alisema uchumi wa wakulima wa wilaya hiyo utapanda kwa kiasi kikubwa baada ya msimu wa mavuno na kwamba, ukipita kwenye maeneo ya Hanang’ utaona mazao ya kijani shambani. Darema alisema matrekta hayo ya mikopo yanauzwa kwa Sh45 milioni hadi Sh35 milioni, mengine yanauzwa hadi Sh25 milioni kwani Serikali imechangia Sh10 kila trekta.    

0 comments:

Post a Comment