Tuesday, July 29, 2014

On 1:57 AM by Shambani Solutions   No comments
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru imenza ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kukoboa mpunga pamoja na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi mpunga tani 1,500.Mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha Sh1 bilioni na kuwasaidia wananchi kuongeza thamani ya mchele hivyo kuweza kuuza katika supermakert kubwa na kuinua pato la wakulima wa zao hilo.Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya kutembelea kiwanda hicho Afisa Kilimo Wilaya ya Tunduru, Chiza Marando alisema kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kukoboa tani 30 kwa siku
Alisema,mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa halmashauri na vikundi 13 vya wakulima wa umwagiliaji wa zao la mpunga ambao wamejiunga katika chama cha ushirika cha umwagiliaji ambapo katika awamu ya kwanza ya mradi wamejenga kiwanda hicho ambacho kitafungwa mashine za kisasa zenye uwezo wa kukoboa mpunga daraja la kwanza na kutoa mawe yote.
“Kwa sasa juhudi mbalimbali zinafanywa kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitakuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima wa mpunga na kikimalizika tutaingia katika awamu ya pili ya kujenga maghala mawili ya kuhifadhia mpunga,”alisema Marando.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Chande Nalicho alisema lengo la kujengwa kwa kiwanda hicho ni kuwasaidia wananchi wa Tunduru kupata soko la uhakika la mchele ilikuwaongezea kipato zaidi ambapo serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata kipato kwa kutumia mazao mengine ikiwemo karanga, mchele, alizeti na kwamba viwanda vinne vya kusindika zao hilo vimejengwa badala ya kutegemea zao moja la korosho ambalo soko lake likiyumba wananchi wanaishi maisha magumu.
Aidha, Nalicho amewaonya wakulima kutochagua viongozi wa ushirika wenyetabia ya ubadhirifu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu bali wachague viongozi waaminifu ambao wanauchungu na wakulima iliwaweze kusaidiana na serikali kuwaletea maendeleo badala ya kuwanyonya na kuwafilisi wakulima.

0 comments:

Post a Comment