Sunday, December 15, 2013
On 1:07 PM by Shambani Solutions No comments
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe amesema Serikali
itawasaidia wakulima wadogo wanawake ili kuleta tija katika sekta ya
kilimo.
Maembe alisema hayo jana wakati wa kumtangaza mshindi wa Shindano la Mtandao la Mama Shujaa wa Chakula.
Alisema wanawake wamekuwa viungo muhimu katika
maendeleo ya familia na ni muhimu kuwasaidia wakulima wadogo kwa ajili
ya maendeleo ya taifa.
“Watu wanahitaji chakula kila siku, asilimia kubwa
ya wazalishaji wa chakula ni wakulima wadogo ambao kazi zao huleta tija
kwa sababu watu wanahitaji kula ili kufanya kazi na kuleta maendeleo”,
alisema.
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula mtandaoni ni sehemu ya kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam.
Shindano hilo liliandaliwa na mmoja wa mabalozi wa kampeni ya Grow, Shamim Mwasha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment