Saturday, November 9, 2013

On 1:08 AM by Shambani Solutions   No comments
 Wakati tunaelekea kwenye kipindi cha kuanza kupanda na kuotesha miti mipya ya msimu wa 2014- 15 ambao huanza rasimi mwezi wa 12 wa kila mwaka, watu wengi sana walitutumia email  na kutupigia simu, kulizia taratibu za  kupata maeneo  ya  kupata mashamba, na wale wenye mashamba walitupgia kuulizia namna ya kupata miche  ama kununua mashamba yenye miti zaidi ya yale waliyonayo kwa sasa. Makala hii fupi inafafanua kwa undani zaidi, hii ni kwa faida ya watu wengine.

Unaweza kununua mashamba yenye miti tayari kwa mchanganuo ufuatao:

Miti pamoja na ardhi: Miti ya mwaka mmoja  =  600,000 Miti ya miaka 2 = 700,000 hadi 800,000 (bei zinatofautiana kutokana
na ‘location’ yalipo mashamba husika).

Mashamba ambayo hayana kitu (yasiyo na miti) huuzwa kwa shilingi laki 200,000/ kwa ekari. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni shilingi laki mbili kwa ekari moja.

Hata hivyo unaweza kupata mashamba haya yenye miti kwa bei za chini zaidi ya hizo kutegemea na wenyeji unaokutana nao pamoja na maeneo husika na idadi ya ekari unazonunua.

Ukinunua shamba tupu itakugharimu wastani wa shilingi laki tatu hadi nne katika kuandaa shamba hadi kupanda. Kwa ushauri wetu tunakushauri kama ukiweza ni vema kutafuta mashamba yenye miti tayari, ununue. HII itakusaidia kuepusha usumbufu wa kuandaa na kupanda hadi ishike ardhini. Ukishanunua shamba iwe ni kutoka kwetu ama kwa wenyeji, kunakuwa na ‘documents’ ambazo zinatolewa na serikali ya kijiji husika kwa idhini ya kamati ya ardhi ya kijiji.

Kwa upande wetu (ikitokea unanunua kutoka plots za kampuni) mara zote management fee tunaijumlisha katika bei ya manunuzi. Kitu ambacho utaendelea kufanya ni kugharimia uhudumiaji wa shamba ambao una shughuli kubwa mbili; 1) Kuproon-wastani wa shilingi laki moja kwa ekari na inafanyika mara mbili hadi tatu kuanzia kupanda hadi kuvuna. 2) Kutengeneza njia kuzunguka shamba na inafanyika kila mwaka na ni wastani wa shilingi elfu sitini kwa ekari moja.

Miti ipo ya aina tofauti. Kwa hapa Iringa kuna miti ya aina mbili inayostawi; ya (nguzo na mbao) iitwayo milingoti naya (karatasi na mbao) iitwayo Pines. Hii ya milingoti inachukua muda mfupi zaidi kukua (wastani wa miaka mitano hadi saba ikiwa ni kwa matumizi ya nguzo na mirunda hutumia miaka miwili hadi mitatu) na pines ambayo ni maalumu kwa ajili ya mbao na kutengenezea karatasi inachukua miaka 7 hadi kumi mpaka kuvunwa.

Ekari moja inachukua miche 500 mpaka 600 na ‘survival rate’ ya aina zote mbili nilizokutajia ipo asilimia 80%.

Uvunaji upo wa aina mbili. Unaweza kuamua kuuza miti kama miti (yaani magogo) ambapo kwa miti hii ya nguzo kwa mti mmoja uliokomaa vizuri unauzwa kuanzia 20,000 na kuendelea. Kwa upande wa miti ya mbao na karatasi mti uliokomaa vizuri unauzwa kuanzia 20,000 na kuendelea (ingawa hii pia inaamuliwa na ‘location’ ya shamba. Shamba linapokuwa mahali kusikofikika bei ni ndogo zaidi). Namna ya pili ya uvunaji ni kuvuna mwenyewe kwa maana ya ama kupasua mbao au kutengeneza nguzo za umeme za kuuza. Katika hii ‘option’ ya pili ya uvunaji inakulazimu uwe katika biashara kamili ya mbao kwa sababu utahitaji mashine, leseni, vibali na taratibu nyingine.

Hadi sasa tunavyoongea, hali ya soko la mbao na nguzo/mirunda liko juu sana na demand ni kubwa kuliko supply. Nadhani unatambua kuwa mahitaji ya bidhaa za miti yameongezeka kwa kasi sana miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika na wataalamu wakiwemo SUA wanatueleza kuwa soko la bidhaa za misitu (mbao, nguzo n.k) litaendelea kupanda bila kushuka kwa miaka 25 ijayo kuanzia mwaka 2010. Kama wawekezaji tunakuwa positive katika hilo ijapokuwa hatuachi kuweka tahadhari ya risks (ikiwemo market changes) kama ambavyo ni kawaida kwa biashara yeyote duniani

Ninaamini nimekupa ufafanuzi mzuri na mahali popote ambapo utakuwa hujapaelewa ama unahitaji ufafanuzi zaidi usisite kuwasiliana nami. Ni furaha yangu ukisaidika na kufanikiwa.

Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara katika makala zangu; ni kwamba muda wa kulalamika lalamika umekwisha. Mazoea na utamaduni wa watanzania wengi kudhani kwamba tunaonewa wakati wote haujatusaidia mpaka hapa kwa jinsi hii hakuna sababu ya kuendelea nao.

Mtindo wa kuishi maisha ya kutaka kuhurumiwa yanatupotezea muda wenye thamani. Tumekuwa tukilalamika kuwa wageni (wanaokuja kwa jina la wawekezaji) wanatupora ardhi; lakini tusichokitafakari ni hiki, “Mimi kama mtanzania kwa nafsi yangu na kwa uwezo wangu nimefanya nini cha maana katika ardhi ninayoweza kuipata hapa nchini ama ninayomiliki?”.

Imeandikwa na
: Meshack Maganga
E: meshackmaganga@gmail.com
P: 0767 48 66 36 ama 0713 48 66 36.
W: http://freshfarm.co.tz 

0 comments:

Post a Comment