Monday, September 16, 2013

On 11:36 PM by Shambani Solutions   No comments
Dar es Salaam. Wataalamu wa sekta ya pamba nchini, wamesema kama wakulima wa pamba watasaidiwa kuendeleza kilimo cha mkataba kilimo hicho kitabadilisha maisha yao.
Mkaguzi wa Pamba katika Wilaya ya Bunda, Igore Manonga, alisema kuanzishwa kwa kilimo cha mkataba, kumeleta faida kwa wakulima wa zao hilo na kwamba kuna haja ya kukiendeleza.
“Kabla ya kuanzishwa kwa kilimo cha mkataba, uzalishaji wa pamba wilayani Bunda ulikuwa wastani wa kilo 250 mpaka 300 kwa ekari, lakini baada ya kuanzishwa katika msimu wa mwaka 2010 uzalishaji uliongezeka na kufikia kilo 300 hadi 600 kwa ekari moja,” alisema Manonga.
Alisema baadhi ya wakulima wanazalisha hadi kilo 1,000 kwa ekari yakiwa ni matokeo ya kilimo cha mkataba.
Mkaguzi wa Pamba wilayani Butiama, Alphone Ngewagale, alisema karibu kila wilaya yenye mradi wa kilimo cha mkataba, uzalishaji wa zao hilo kwa ekari umeongezeka kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Post a Comment