Sunday, August 11, 2013

On 4:51 PM by Shambani Solutions   No comments
Waziri wa Kilimo na Ushirikia Mh Chirstopher Chiza
Chiza alitoa kauli hiyo katika Viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma wakati akizundua maonyesho ya Wakulima Kitaifa Nane Nane iliyokuwa na kauli mbiu ya ZALISHA MAZAO YA KILIMO NA MIFUGO KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO. na kuwataka vijana kuandamana maelfu kwa maelfu kama wanataka mabilioni ya fedha maarufu kama mabilioni ya Kikweteili mradi wawe tayari kuyatumia kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kilimo

Waziri huyo alisema, maandamano ya vijana hata kama yatakuwa kwa maelfu lakini yakilenga kupata fedha kwa shughuli za kilimo, hayatakuwa na madhara na atayapokea.
“Kilimo ni ajira kwa vijana, kama wataandamana kwa kudai kilimo niko tayari kuwapokea kuliko kama wataandamana kwa kudai ajira na mambo mengine, nataka vijana wapewe fedha na ardhi ili wajikombe kwa shughuli zao,” alisema Chiza.
Kutokana na kauli hiyo, aliwaita wakuu wa wilaya za mikoa ya Dodoma na Singida ambao waliapishwa mbele yake ili kujua kama wanamipango madhubuti katika wilaya zao kwa ajili ya kuwapa ardhi vijana.

Wakuu wa wilaya zote waliahidi mbele yake kuwa wataendeleza utaratibu wa kutenga ardhi kwa ajili ya vijana isipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Lephy Gembe, ambaye alisema kuwa Sera za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ni kikwazo kwa wilaya yake.
Kwa upande mwingine Chiza alisema ni wakati sasa wa Tanzania kuondoka katika kilimo cha kujikimu na kwenda katika kilimo cha uzalishaji zaidi ili kuinua tija. Alisema Sera yake ni kuzalisha kwa wingi na kutafuta masoko na si kuzuia mazao ya Tanzania kuvuka kwenda nje ya nchi kama inavyofanyika kwa sasa.
Akizungumzia gharama za maonyesho ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau, alisema “hatuwezi kufuta maonyesho ya Nanenane kwa kuwa yana umuhimu wa pekee na faida kwa wakulima wetu.” Alisema kuwa malalamiko kuwa maonyesho hayo yanagharimu fedha nyingi si kweli na kama kuna ukweli wa aina yoyote ipo haja ya kuangalia namna ya kupunguza gharama lakini si kuyaondoa maonyesho hayo. Hata hivyo, aliwaagiza viongozi kufanya kwa vitendo ili waweze kuendana na kauli mbiu kuliko kutofanya hivyo na kufanya kauli mbinu hiyo kuwa ni nyimbo za kasuku.



0 comments:

Post a Comment