Friday, February 8, 2013

On 2:56 AM by Shambani Solutions   No comments
Shamba la Mpunga Mbalizi
BAADHI ya wakulima wa zao la mpunga Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali kuwafikishia wataalam wa kilimo, ili waweze kuwapatia elimu ya kilimo bora cha kisasa ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao hili na kupata soko la uhakika la ndani na nje kwa kutumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.
Wakizungumza na gazeti hili jana katika kata ya Igurusi,walisema elewa mdogo wa kutozingatia kanuni bora za kilimo ni chanzo cha kutopata mazao mengi ya chakula na biashara hususan ukosefu wa dhana za kisasa za kilimo,ambapo baadhi yao bado wanaendelea kutumia kilimo cha ng’ombe na punda.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima,Amos Matanana alisema uelewa mdogo wa kuzingatia kanuni bora za kilimo ni chachu kwao na kwamba ni wakati wa serikali sasa kuwasaidia wakulima vijijini kufikiwa na wataalamu wa kilimo ili waweze kupatiwa elimu kupanda mazao kwa kuzingatia utaalam wa kilimo bora na cha kisasa.

Aidha alisema kuwa wakulima wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi hususan kipindi cha msimu wa kilimo, ukosefu wa skimu za umwagiliaji na kwamba hali hiyo imekuwa ikichangia wakulima kutopata mazao mengi katika msimu wa mavuno.

Alisema wanaiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwafikishia mikopo ya matrekta madogo (powertiller) ili waweze kuzalisha zao hilo kwa wingi na kupata soko la uhakika litakaloweza kumkwamua kiuchumi mkulima mmoja mmoja kiuchumi.

0 comments:

Post a Comment