Sunday, February 24, 2013

On 2:41 AM by Shambani Solutions   No comments


NDG PHILEMON LUHANJO - KATIBU MKUU KIONGOZI ALIYESTAAFU
Nimeitumikia serikali katika nyadhifa mbalimbali kwa muda wa miaka 35 tangu mwa 1977 hadi mwa 2011 nilipostaafu kipindi hicho chote nilikuwa nafanya kazi za ofisini lakini nilipenda sana siku ntakapostaafu nifanye kazi za tofauti na kazi za makaratisi, na sasa baada ya kustaafu nimeamua kujishughulisha na kilimo kama shughuli yangu rasmi.

Napenda sana kilimo na mimi ni mmoja wa watu walioanzisha kauli mbiu ya KILIMO KWANZA nilipokuwa katika baraza la taifa la biashara kama mwenyekiti wa kamati ya utendaji, tulianzisha kauli mbiu hiyo kwa kuwa kila jambo linategemea kilimo na pia kilimo ndo uti wa mgongo wa taifa letu na kinaajiri asilimia 80 ya watanzania wote. Maneno hayo yalisemwa na aliyekuwa katibu mkuu kiongozi ndg Philemon Luhanjo akiwa katika mshamba yake ya chai mkoani njombe

Akizungumzia namna anayotumia mda wake mwingi kwa sasa kujishughulisha na kilimo anasema tangu aingie shambani mwaka jana amekuwa shambani hadi leo (February 20 2013) baada ya hapo ntarudi dsm kidogo kwa likizo kisha ntarudi tena shambani kuhudumia mashamba yangu

Luhanjo aliendelea kusema, ameamua kujishughulisha na kilimo kwa kuwa anakifahamu vizuri na kupitia makala hii anapenda kuhamasisha watumishi mbalimbali walio maofisini kutokipuuza kilimo badala yake wageukie kilimo maana kina faida kubwa sana

Aliendelea kutoa motisha chanya kwa wastaafu wengine wamtembelee ili wajifunze kutoka kwake maana wastaafu wengi hukimbilia kufanya biashara zinaoweza kuwalipa kwa muda mfupi na kukiacha kilimo kwa kuhofia uhaba wa mvua na sababu zingine mbalimbali ikiwemo kukitazama kilimo kama shughuli wa watu waliopoteza matumaini, wasio na elimu na waliokosa shughuli zingine za kufanya

Luhanjo alieanza kujishughulisha na kilimo mwaka 2010 kabla ya kustaafu hakusita pia kueleza changamoto mbalimbali alizokutana nazo mpaka sasa kama vile uhaba wa mvua, wadudu waharibifu, soko kutokuwa la kuaminika hasa pale wakulima wanapozalisha kwa wingi sana bei za mazao hushuka na kupunguza faida kwa mkulima

Pia aliishauri serikali kuanzisha utaratibu wa maafisa kilimo kusomea zao moja ili ajikite kisawasawa katika kulifahamu zao hilo hatimaye afisa huyu wa kilimo aweze kuwasidia wakulima kwa ufanisi

Fuatilia habari hii kwa kina kupitia: http://www.habarileo.co.tz/index.php/nyota/9220-philemon-luhanjo-ktaibu-mkuu-kiongozi-aliyegeuka-mkulima

0 comments:

Post a Comment