Thursday, January 24, 2013

On 3:20 PM by Shambani Solutions   No comments

Maneno hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Njombe Mh Sarah Dumba alipohudhuria mafunzo ya siku moja kuhusu Ukanda wa kilimo kusini mwa Tanzania (SAGCOT), 

Dumba alisema kufikia 2030 zaidi ya watu 420000 wanatarajiwa kupata ajira ya uhakika ambapo kwa kuanzia mpango huo utatekelezwa katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Rukwa, Mbeya, Njombe na maeneo mengine yaliyo karibu na barabara kuu, bandari, usafiri wa anga na maeneo yanayofikika kwa haraka zaidi na kwa mwaka mzima

Katika kuendeleza Mpango huo mamlaka ya uendelzaji wa Bonde la Mto rufiji(Rubada) imepewa jukumu la kutafuta wawekezaji kwa mfumo wa ushirikishwaji kati ya wanavijiji, serikali na wawekezaji hao,

Aliendelea kusema “ Bonde la Kilombero lina hekta 300,000 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji huku mbarali likiwa na zaidi ya hekta 200,000 lakini zinazotumika ni chini ya asilimia mbili

Alisema Mafanikio ya rubada katika kutekeleza mpango wa SAGCOT  yanalenga kuwatoa wakulima katika kilimo cha mazoea na kulima kwa faida zaidi ambapo kufikia mwaka 2013 jumla ya hekta  350,000 zitakuwa zimeendelezwa na hali hiyo itaweza kutoa ajira kwa wananchi zaidi ya 420,000 wengi wao wakiwa vijana

Mpango wa SAGCOT  ulianzishwa katikati ya mwaka 2010 ikiwa na lengo la kuongeza thamani ya mazao husika kwa kuweka viwanda, masoko na miundombinu ya uhakika karibu na maeneo ya kilimo ili kuboresha uzalishaji na baadae kuleta faida kwa mkulima mmojamoja na hatimaye nchi yote kufaidia

Mratibu wa mpango huo wilayani hapa Weisy Wikedzi alitaja baadhi ya maadhimio yaliyofikiwa na madiwani wa wilaya ya Njombe mara baaday ya mafunzo hayo ni kutilia mkazo katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, kilimo cha mahindi, viazi, maua, alizeti na nyanya kulingana na hali ya hewa ya maeneo husika.

0 comments:

Post a Comment