Tuesday, January 22, 2013

On 10:27 AM by Shambani Solutions   No comments



Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia chakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

MBEGU BORA ZA MUHOGO
       i.            Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
                                 ·         I. .   Naliendele   -  Hii uzaa zaidi ya tani 19 kwa mwaka kwa hector moja na inaweza kuvunwa kuanzia miezi  9 tangu ipandwe 
                                                              ii .     Kiroba - Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

MBINU BORA ZA KILIMO CHA MUHOGO
  • ·        UANDAAJI WA SHAMBA
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
- Kufyeka shamba
- Kung’a na kuchoma visiki
- Kulima na kutengeneza matuta

  • ·        UCHAGUZI WA MBEGU BORA ZA KUPANDA

Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.

  • ·        UPANADAJI

Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
-   Kulaza ardhini (Horizontal)
-  Kusimamisha wima (Vertcal)
-  Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

  • ·        UREFU WA KIPANDE CHA SHINA CHA KUPANDA:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

  • ·        NAFASI YA KUPANDA:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita
  • ·        PALIZI:
-          Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na
            magugu
yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo    haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
-          Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
-          Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
-          Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

  • ·        UVUNAJI:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.



  • ·        USINDIKAJI BORA

Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
-          Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
-          Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
-          Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji
-          Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
-          Kwa kutumia mashine aina ya chipper
-          Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

  •  MATUMIZI YA MUHOGO
- Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
- Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga
wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k
Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

0 comments:

Post a Comment