Tuesday, January 15, 2013

On 6:19 AM by Shambani Solutions   5 comments


Sakata hilo lilijitokeza juzi katika mkutano wa wadau wa kilimo ulioandaliwa na Baraza la Kilimo la Taifa (ACT), wakulima walikuja juu wakishangaa benki hiyo kutoanza kazi licha ya ahadi ‘kibao’ zilizokuwa zikitolewa.
Akichangia katika mkutano huo, Alloyce Shemweta kutoka Kikundi cha Wakulima wa Michikichi, mkoani Kigoma alihoji ukimya wa baraza hilo kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo licha ya ahadi za mara kwa mara zilizokuwa zikitolewa.

Shemweta alilalamika zaidi na kudai kwamba wakulima waliahidiwa benki ya kilimo  ingeanzishwa Desemba mwaka jana lakini hatujaiona ikianzishwa  na kuhoji tatizo nini? Kauli hiyo iliungwa mkono na washiriki wa mkutano huo waliotaka kufahamu mchakato wa uanzishwaji wa benki hiyo ulipofikia.

Akitoa ufafanuzi, Mwenyekiti ACT, Salum Shamte, alisema mchakato wa kuanzishwa kwa benki hiyo, umefikia katika hatua ya kupata wakurugenzi wa bodi wa benki. Shamte alisema jumla ya Watanzania 9,000 wameomba nafasi za ukurugenzi wa bodi ya benki hiyo inayohitaji wajumbe saba tu.

“Benki inahitaji wajumbe saba tu wa bodi lakini wajumbe walioomba nafasi hiyo ni zaidi ya 9,000. Hivyo BoT na Wizara ya Fedha wanachambua maombi hayo ili kuwapata wajumbe hao,” alisema Shamte.

Ingawa Shamte hakusema benki hiyo itaanza lini, lakini alisifu juhudi za Serikali kwa kutenga Sh100 bilioni katika bajeti yake ya mwaka 2012/13 kwa ajili ya kuianzisha. Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu jana hakupatikana kuzungumzia suala hilo kwa kuwa simu yake ya kiganjani, haikuwa inapatikana.
Kuanza kufanya kazi kwa benki hiyo itakuwa ukombozi kwa wakulima ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia ukosefu mikopo ya kilimo.

Wakulima hao wamekuwa wakishindwa kupata mikopo kutoka katika benki mbalimbali kwa sababu za kukosa dhamana na riba kubwa zinazotozwa.

5 comments:

  1. katika hili serikali ni lazima ihakikishe inaweka mazingira yatakayowawezesha wakulima kupata mikopo ktk taasisi za fedha ili waweze kukuza uzalishaji

    ReplyDelete
  2. wananchi wakiwa wanafuatilia masuala yanayo wahusu hivi hata watendaji wataacha uvivu sababu watajua wasipofanya wataulizwa

    ReplyDelete
  3. Tatizo benki kama hiyo haitawasaidia wakulima wadogo,itawajali wakulima wakubwa

    ReplyDelete
  4. ni kweli mdau na hilo ndo tatizo la msingi la taasisi zetu za fedha haziwwamini sn wakulima hasa wadogowadogo hali inayopelekea kuzorota kwa kilimo nchini

    ReplyDelete
  5. yaani hiyo bank ni muhimu sana ikawepo wadau japo kuna watu hawaitaki na wanatumia kivuli cha kuanza kutoa mikopo ya bei nafuu kwa wakulima ili pesa zote zipitie humo

    ReplyDelete