Wednesday, January 9, 2013

On 4:37 AM by Shambani Solutions   No comments
Sakata la uuzwaji wa ndege tatu za taasisi ya kilimo anga jijini arusha lachukua sura mpya hasa baada ya waziri mwenye dhamana Mh Chiza kuingilia kati na kuagiza kusimamisha uuzaji wa ngede iliyobaki.Pia Mh Chiza alienda mbali zaidi na kuagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini bei iliyotumika kuuza ndege hizo, zimeuzwa kwa kampuni gani na ziko wapi kwa sasa ili hatua ziweze kuchukuliwa, pia Waziri Chiza alitoa maagizo hayo baada ya kusikitishwa na hali ya taasisi ya kilimo anga pale alipotembelea tasisi hiyo juzi na kukutana na mhandisi mkuu wa kituo hicho Gideon Mugusi.
Mbali na hilo pia mhandisi Mugusi alielezea na matatizo mengine yanayokikabili kituo ikiwemo kukimbiwa na marubani wake 12 kwa sababu ya kutafuta masilahi zaidi sehemu nyingine, kukosekana kwa fedha za kendesha shughuli za kila siku.

Mwishoni katika kuonesha serikali ina mpango wa kufufua kituo hicho Mh Chiza aliwaambia wadau kwamba serikali imetenga jumla ya Tsh bil 1.5 ili kununua ndege zingine mpya ili zoezi la udhibiti wa wadudu waharibifu liendelee kama ilvyokuwa zamani 
 Kwa taarifa zaidi tembelea link hii:

0 comments:

Post a Comment