Thursday, January 10, 2013

On 1:08 PM by Shambani Solutions   No comments
Mbunge wa Viti maalum kupitia CHADEMA mkoani manyara Mh Paulina Gekul amewaonya mawakala wa pembejeo za kilimo wanawahujumu wakulima kwa kuwasainisha wakulima kupata mbegu na mbolea na badala yake wanawapa mbegu tu na wanaingia mitini na mbolea katika kipindi hiki cha kilimo na kuwataadharisha mawakala hao kwamba mda wa kuendelea kufanya hivyo umeisha 

Mh. Gekul alifichua hujuma hiyo kupitia mtandao wa facebook(babati forum) na kuongeza ya kuwa malalamiko ni mengi na ameshayafikisha kwa mkuu wa wilaya ya babati ambaye ameahidi kulishughulikia kwa karibu maana yeye ndo mhusika wa hili swala katika eneo hili

Mh. Gekul aliandika “Kwa wale wadau wa kilimo babati,,,wananchi wengi wamekuwa wakiniletea malalamiko juu ya tabia ya mawakala wa pembejeo za kilimo wanaowasignisha wananchi fomu za mbolea na mbegu,lakini baadae wanawapa wananchi mbegu tu,na wao wanabaki na mbolea,hii ni hujuma kubwa na haitakubalika,wananchi wa bermi,bonga wameniletea tatizo hili,nimeshalifikisha kwa Dc,amelipokea na analishughulikia,maana yeye ndie muhusika kwa hili, kama kuna tatizo kama hili kwenye maeneo mengine naomba tuwasiliane mapema ili wananchi wasnyonywe na kuonewa na mawakala mafisadi,”  

Mwisho Mh. Gekul ameomba wananchi mbalimbali wenye matatizo kama hayo wawasiliane naye ili waweze kutafuta suluhisho kwa pamoja

0 comments:

Post a Comment