Friday, July 19, 2013
On 10:30 AM by Shambani Solutions No comments
Kwa kutambua information gap katika upatinakanji wa taarifa mbalimbali za msingi shambani solutions inapenda kuwataarifu ya kwamba serikali ya Tanzania kupitia mfuko wa Mendeleo ya vijana imeanza kazi ya kutoa
mikopo kwa vikundi vya vijana ili wawekeze na
waendeleze miradi yao ya kijasiriamali kwa lengo la kusaidia vijana kutimiza
ndoto zao.
Takwimu zinaonyesha kuwa kuna jumla ya Vijana milioni 16,195,370
ambapo takribani vijana 1,200,000 humaliza elimu ya vyuo mbalimbali kila mwaka
na kati yao ni vijana 200,000 huajiriwa kwa mwaka.
Pia Ikumbukwe kuwa Vijana wanachukua asilimi 68 ya nguvu kazi ya
Taifa lakini takwimu zinaonyesha kuwa upungufu wa ajira kwa Vijana ni asilimia
14.4.
Hivyo serikali imetoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo
ambayo haimuhitaji mkopaji kuwa na dhamana isiyo hamishika bali kuwa na
uaminifu wa kurejesha mkopo huo utakaotolewa kupitia vyama vya kuweka na kukopa SACCOS.
Hivyo Vijana mnashauriwa kujiunga katika vikundi na kufanya
mawasiliano na Maafisa Vijana katika Halmashauri zenu ili kujua taratibu za
kupata mikopo hiyo.
Zingatio kwa mkopo huu
Walengwa
Vijana wenye umri kati ya miaka 15-35
Riba
Asilimia kumi kwa mwaka (10%)
Vijana wenye umri kati ya miaka 15-35
Riba
Asilimia kumi kwa mwaka (10%)
Mikopo itatolewa kupitia Saccos za Vijana.
Cha msingi ni kujiunga katika vikundi, kujisajili, kutengeneza mchanganuo wa biashara na mwishowe mnakwenda
halmashauri kuomba mikopo hiyo, pale halmashauri utakutana na maafisa maendeleo
wa kata mitaa na wilaya ambapo watakupa utaratibu kamili ili upate mkopo huo,
cha msingi wewe jitambulishe tu kwamba umekwenda pale kwa ajili ya MFUKO WA
MAENDELEO YA VIJANA
Pia tembelea: http://apf-tanzania.ning.com/profiles/blogs/youth-development-fund-ydf-targets-youth-in-groups
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment