Wednesday, June 5, 2013
On 2:58 PM by Shambani Solutions No comments
WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amewataka wakazi wa wilaya mpya ya Mlele mkoani Katavi walime mazao mbadala ya biashara kama alizeti, karanga na ufuta kwa sababu yanachukua muda mfupi na hivyo kuleta kipato cha haraka.Ametoa
wito huo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nsenkwa mara baada ya
kuweka jiwe la msingi kwenye zahanati ya kijiji hicho akiwa katika siku ya pili
ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani Mlele, mkoani Katavi.
Aliwataka
wakazi hao waangalie ufugaji nyuki kama fursa ya kipekee kwa sababu mkoa huo umejaliwa kuwa na misitu mingi na unaweza kuongeza kipato cha mkoa wao. “Asali ni dawa, asali ni chakula, asali ni biashara na ina soko hapa nchini hadi nje ya nchi. Changamkieni fursa hii, ongezeni uzalishaji wa asali na nta,” aliongeza. Aliwashauri
pia waangalie uwezekano wa kulima miembe ya kisasa kwa sababu inazaa kwa wingi na katika kipindi kifupi mno. “Hii miembe yenu inazaa maembe 10-20 kwa mwaka lakini ya kisasa inazaa hadi maembe 10,000, ikiwa chinichini tu,” alisema.
Akihimiza kanuni bora za kilimo, Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Mlele aliwataka waachane na kilimo cha matuta na badala yake watumie kilimo cha sesa. “Ekari moja ya mahindi inapaswa ikupatie magunia 20-25 ya mahindi, sasa wewe unalima ekari tatu na kuvuna magunia 10, sababu kubwa ni nafasi zinazopotea kwenye miraba ya matuta, alisema. “Ni lazima tuondokane na kilimo hiki kwa sababu hakina tija na tena kinatumia nguvu nyingi na kupoteza eneo kubwa ambalo lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment