Thursday, January 24, 2013
On 3:20 PM by Shambani Solutions No comments
Maneno hayo yalisemwa
na mkuu wa wilaya ya Njombe Mh Sarah Dumba alipohudhuria mafunzo ya siku moja
kuhusu Ukanda wa kilimo kusini mwa Tanzania (SAGCOT),
Dumba alisema kufikia
2030 zaidi ya watu 420000 wanatarajiwa kupata ajira ya uhakika ambapo kwa
kuanzia mpango huo utatekelezwa katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Rukwa,
Mbeya, Njombe na maeneo mengine yaliyo karibu na barabara kuu, bandari, usafiri
wa anga na maeneo yanayofikika kwa haraka zaidi na kwa mwaka mzima
Katika kuendeleza
Mpango huo mamlaka ya uendelzaji wa Bonde la Mto rufiji(Rubada) imepewa jukumu
la kutafuta wawekezaji kwa mfumo wa ushirikishwaji kati ya wanavijiji, serikali
na wawekezaji hao,
Aliendelea kusema “
Bonde la Kilombero lina hekta 300,000 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji huku
mbarali likiwa na zaidi ya hekta 200,000 lakini zinazotumika ni chini ya
asilimia mbili
Alisema Mafanikio ya
rubada katika kutekeleza mpango wa SAGCOT
yanalenga kuwatoa wakulima katika kilimo cha mazoea na kulima kwa faida
zaidi ambapo kufikia mwaka 2013 jumla ya hekta
350,000 zitakuwa zimeendelezwa na hali hiyo itaweza kutoa ajira kwa
wananchi zaidi ya 420,000 wengi wao wakiwa vijana
Mpango wa SAGCOT ulianzishwa katikati ya mwaka 2010 ikiwa na
lengo la kuongeza thamani ya mazao husika kwa kuweka viwanda, masoko na
miundombinu ya uhakika karibu na maeneo ya kilimo ili kuboresha uzalishaji na
baadae kuleta faida kwa mkulima mmojamoja na hatimaye nchi yote kufaidia
Mratibu wa mpango huo
wilayani hapa Weisy Wikedzi alitaja baadhi ya maadhimio yaliyofikiwa na
madiwani wa wilaya ya Njombe mara baaday ya mafunzo hayo ni kutilia mkazo
katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, kilimo cha mahindi, viazi, maua, alizeti
na nyanya kulingana na hali ya hewa ya maeneo husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment