Sunday, January 27, 2013
On 6:47 AM by Shambani Solutions 2 comments
1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana katika
Ofisi za kilimo za Halmashauri za Wilaya na Makao makuu ya Mfuko wa Pembejeo,
jijini Dar-es-salaam na katika tovuti ya wizara ya kilimo.
2. Fomu za maombi zilizojazwa na
kuambatanishwa na vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa/kuidhinishwa na Afisa
Kilimo wa Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya husika
na baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo.
3. Mikopo ya kununua
matrekta inatolewa na Mfuko wa Pembejeo, baadhi ya benki na taasisi za fedha na
SCCULT (T) Ltd. kwa niaba ya
Mfuko, mwombaji sharti atimize yafuatayo:-
i)
Awe na dhamana yenye hati miliki
isiyohamishika iliyoandikishwa kwa jina la mwombaji.
ii)
Awe na shamba binafsi
lisilopungua hekta 50 na awe tayari kutoa huduma ya kuwalimia wakulima wengine
iii) Awe tayari kutekeleza masharti yote ya Mfuko wa Pembejeo au
taasisi ya fedha na SCCULT yanayohusu mkopo wa ununuzi wa trekta jipya.
iv) Awe tayari kulipa asilimia moja (1%) ya mkopo kama gharama
za nyaraka za mkopo na kusajili trekta kwa pamoja kwa jina lake
na Mfuko
v)
Riba inayotozwa ni asilimia
nane (8%) na marejesho hufanyika kwa muda wa miaka mitatu kila baada
ya miezi mitatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
hii haijakaa powa coz inalenga wakulima wakubwa na si wakulima wadogo.
ReplyDeleteWakulima wadogo wafanye
ReplyDeletenini?