Thursday, August 21, 2014

On 12:44 PM by Shambani Solutions   No comments
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa wito kwa watumishi wa Serikali kutoingiza siasa katika kuendeleza sekta ya kilimo Kanda ya Ziwa.
Akihutubia katika maonyesho ya Sikukuu ya Nane nane Kanda ya Ziwa yanayofanyika kwa mara ya pili Viwanja vya Nyamh’ongolo jijini Mwanza,Pinda alisema kuwa msingi wa kauli mbiu ya mwaka huu isemayo; Matokeo makubwa sasa: kilimo ni biashara, inaweza kutimia katika siasa haitaingia katika sekta ya kilimo.
“Naomba sana siasa isiingie katika sekta ya kilimo, ila mkitaka kilimo kiwanufaishe watu, lazima tuwekeze kwa wakulima wadogo pia tuingize matumizi ya teknolojia na siyo siasa kwani msingi wa kauli mbiu hii ni mkulima alime, ale ila akiba kidogo auze,”alisema Waziri Mkuu.
“Nimeongea na wawekezaji kutoka China ili kuanzisha viwanda vya kutengeneza matrekta nchini badala ya kwenda kununua kwao kwani gharama inakuwa kubwa, wamekubali huku kampuni nne zikijitokeza na tumekubaliana mpaka September 2015 wawe wametengeneza matrekta 4,000 kwa kujenga viwanda Kanda ya Kusini, Kanda ya Kati na Kanda ya Ziwa,”alisisitiza.
Aliongeza kuwa wakulima wanaotumia matrekta kwa Kanda ya Ziwa ni asilimia 62, huku asilimia 24 wakitumia jembe la mkono jambo alilosema linachangia sekta hiyo kutoa mchango mdogo katika pato la taifa.
Pinda alisema kuwa, Tanzania inashika nafasi ya nne Afrika katika uzalishaji wa mahindi na nafasi ya kumi na moja duniani.

0 comments:

Post a Comment