Tuesday, August 19, 2014
On 3:06 AM by Shambani Solutions 4 comments
Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha
moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama
tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la
chini la damu. Pia tango linaaminika kupunguza kiwango cha rehemu,
mafutayenye madhara mwilini, huimarisha misuli na pia husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo.Virutubisho vilivyopo katika tango hutoa nafuu kawa mtu mwenye matatizo
ya ini, kongosho, figo na matatizo katika kibofu cha mkojo.
Watalamu wetu wanatueleza kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana
kama ‘erepsin’ ambacho husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambayo ni
muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini.
Vile vile tango lina kiwango kikubwa cha vitamin C hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa vitamin hiyo, kama vile fizi kuvuja damu, upunguvu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.

Kinga ya Saratani
Pengine faida kubwa kuliko zote unazoweza kuzipata kwa kula tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linalotokana na ukweli kuwa tango lina kiwango kikubwa cha uchachu ‘alkaline’, na kufanya seli za saratani kuwa katika mazingira magumu ya kusambaa mwilini, kwani kwa kawaida seli za saratani haziwezi kuishi kwenye mazingira zenye uchachu. Hivyo ni vyema kujijengea mazoea ya kula tango mara kawa mara ili kujiwekea ulinzi na kinga ya saratani za aina mbalimbali.

Dawa ya magaonjwa ya ngozi
Tangu enzi na enzi tango limekuwa likitumika katika masuala ya urembo wa ngozi. Watu wengi hutumia tango kwa njia mbalimbali kutunza ngozi zao na kupendezesha sura, hata baadhi ya vipodozi visivyo na madhara hutengenezwa kutokana na tango.

\
Ulaji wa tango na unjwaji wa
juisi yake mara kwa mara huondoa matatizo mengi ya ngozi yaliyo ndani na
nje, kama utachukua hatua ya kutumia juisi yake kwa muda wa wiki mbili
hadi tatu mfululizo.
Baada ya matumizi, hakika utakuwa na ngozi nyororo yenye afya kushinda mtu anayetumia vipodozi.
Baada ya matumizi, hakika utakuwa na ngozi nyororo yenye afya kushinda mtu anayetumia vipodozi.
Jinsi ya kuandaa juisi ya tango
Ni rahisi sana kutengeneza juisi ya tango. Chukua tango, katakata
vipande tayari kwa kusaga ama kwa mashine au kwa kutwanga katika kinu
maalumu, kisha changanya na maji masafi ili kupata juisi glasi moja. Unaweza kuweka sukari kiasi kidogo sana au unaweza kuweka asali kijiko
kimoja utapata matokeo mazuri ya haraka kama ukinywa juisi yako asubuhi
kabla ya kula kitu chochote. Ili kutibu matatizo ya ngozi au magonjwa mengine kama tulivyoyaeleza hapo juu, inakupasa kunywa juisi ya tangokwa muda wa wiki mbili au nne mfululizo kisha angalia matokeo yake.
\
Kwa afya njema, jenga mazoea ya kunywa japo mara mbili au tatu kwa wiki, vilevile unaweza kujiwekea mazoea yakula tango kwa njia mbalimbali kama vile kuchanganya na saladi, kachumbali au kulitafuna lenyewe mara kwa mara kwani faida zake ni nyingi mwilini.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Asante sana kwa elimu nzuri ya matumizi ya tango.Mungu akubariki sana.Nitaanza kutumia tango kwa wingi leo
ReplyDeleteNaomba uzidi kutupatia elimu kama hizi,inatusaidia sana
ReplyDeletepamoja sn fatma
ReplyDeletesafi sana ndugu
ReplyDelete