Saturday, February 15, 2014

On 11:21 AM by Shambani Solutions   No comments



Wakulima wa zao la pamba mkoani Mara, wamelalamikia ukosefu wa pembejeo, hususani dawa ya kunyunyuzi zao hilo pamoja na kilimo cha mkataba kwa madai sasa hakiwanufaishi.

Wakulima hao wameyasema hayo juzi mjini hapa, kwenye mkutano uliondaliwa na Bodi ya Pamba. Mkutano huo uliokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa ulishirikisha wakulima wawezeshaji, wadau wa zao hilo, watumishi wa idara ya kilimo, wakurugenzi watendaji wa halmashauri na wakuu wa wilaya zote za Mara.

Katika mkutano huo wakulima hao walilalamikia ukosefu wa dawa za kunyunyuzia zao hilo, ikiwa ni pamoja na baadhi ya kampuni zinazonunua pamba kuwauzia kwa bei kubwa. Walisema dawa ya kunyuzia zao hilo haipatikani na inapopatikana baadhi ya kampuni zimekuwa zikiwauzia kwa bei ya juu ya Sh2,500 badala ya Sh2,000 inayotambuliwa na Serikali kwa kila chupa moja.

Alisema kwa sasa pamba yao imekwishashambuliwa na wadudu waharibifu kutokana na kukosekana kwa dawa.

Akifungua mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula alisema lengo ni kutaka takwimu sahihi zikusanywe.

0 comments:

Post a Comment