Thursday, February 6, 2014

On 11:46 AM by Shambani Solutions   No comments
Wakulima wa chai mkoani Kagera, wameomba mwekezaji wa Kampuni ya Kagera Coffee Ltd, afukuzwe kwa kile wanachodai hana uhusiano mzuri na wakulima.
Walidai hawalipi kwa wakati wakulima wanaomuuzia majani ya chai. Wakizungumza kwenye semina ya kujadili changamoto zinazowakabili hivi karibuni, wadau wa chai Kanda ya Ziwa, walisema mwekezaji huyo badala ya kuendeleza kilimo hicho anazidi kukididimiza. Mwakilishi wa wakulima Mkoa wa Kagera, Yahya Salim alisema wakulima wanaomba mwekezaji huyo afukuzwe kwa sababu hawajali.
Naye Mwenyekiti wa Wakulima wadogo Mkoa wa Kagera, James Rwegoshora alisema bei kubwa ya pembejeo za kilimo imekuwa tatizo kwao, hivyo Serikali iangalie suala hilo. Makamu Mwenyekiti Umoja wa Wakulima Chai Tanzania, Cleophas Mtambuzi alisema lengo ni kuwa na sauti moja.

0 comments:

Post a Comment