Tuesday, August 13, 2013

On 1:20 AM by Shambani Solutions   No comments
Wakazi wa vijiji vya Lumuma na Pwaga, wilayani Mpwapwa, wamedai hawaoni tija kuwa na ofisa kilimo kwani aliyeko hawasaidii kabisa.

Walitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawane wakimtuhumu ofisa kilimo huyo kuwa hayupo tayari kuwatembelea, badala yake huwataka wamfuate nyumbani kwake. Rumambo Elisha, mkazi wa Kijiji cha Munguwi, alisema nia yake siyo kumchongea ofisa huyo lakini nia yake ni kueleza ukweli kwa mustakabali wa maendeleo ya kijiji. Alisema ofisa huyo hajawahi kuwatembelea hata mara moja.

0 comments:

Post a Comment