Wednesday, July 31, 2013

On 2:33 PM by Shambani Solutions   No comments
Mwenyekiti wa Jukwaaa la Katiba - ndugu Deus Kibamba
Mchakato wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi haujamzungumzia mkulima na nafasi yake katika kuleta maendeleo. Maneno hayo yamesemwa na Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania alipokuwa anaongea na wanachama wa Muungano Wa Vikundi vya Wakulima Tanznia(MVIWATA) walipokuwa katika mjadala wa katiba mpya na nafasi ya mkulima katika katiba mpya

Vilevile Kibamba anasema kama ambavyo mkulima amekuwa akipuuuzwa kwa namna mbalimbali, hata Rasimu ya Katiba inayojadiliwa haijaeleza kinaga ubaga nafasi ya mkulima na ushirki wake mzima katika kumiliki uchumi wa nchi

“Tanzania ni nchi ya Wakulima na Wafanyakazi rasimu ya katiba mpya haielezi nchi hii ni ya akina nani, pamoja na kutoeleza, mimi nadhani nchi hii kwa sasa ni ya wafanyabiashara na wawekezaji,” anasema Kibamba. Aliendelea kubainisha kuwa mawazo ya wakulima hao ni muhimu ili haki zao ziweze kuingizwa, badala ya sasa ambazo ‘zimechomekwa’ katika makundi madogo wakati wenyewe ndio kundi kubwa.

Kwa mujibu wa Kibamba, wakulima hao wapiganie ardhi, rasilimali na misitu ambayo ni mambo muhimu kwa wakulima, ili yaweze kuingizwa katika rasimu, badala ya kuishia kuyaona kama mambo ambayo si ya Muungano.

Pamoja na kuikosoa rasimu hiyo, Kibamba anasema walau imeonyesha kuwa inaandaliwa kwa kuwashirikisha wananchi, wakiwamo wakulima na wafanyakazi, na maandalizi yake yanafuata utaratibu wa kisheria, hivyo Katiba itakayopatikana itakuwa halali ukilinganisha na katiba za mwaka 1961, 1962, 1964, 1965 na hii ya sasa ya 1977 kwani hizi katiba ziliundwa na watu wachche na wananchi walitakiwa wajifunze katiba mara baaada ya kupitishwa” aliendelea kusema.

Source; http://www.mwananchi.co.tz/Makala/Kibamba--Rasimu-ya-Katiba-mpya-haimtaji-mkulima/-/1597592/1932746/-/pjxf82/-/index.html

0 comments:

Post a Comment