Friday, July 19, 2013

On 10:30 AM by Shambani Solutions   No comments

Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mfuko wa maendeleo ya vijana. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Kwa kutambua information gap katika upatinakanji wa taarifa mbalimbali za msingi shambani solutions inapenda kuwataarifu ya kwamba serikali ya Tanzania kupitia mfuko wa Mendeleo ya vijana imeanza kazi ya kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana ili wawekeze na waendeleze miradi yao ya kijasiriamali kwa lengo la kusaidia vijana kutimiza ndoto zao. 

Takwimu zinaonyesha kuwa kuna jumla ya Vijana milioni 16,195,370 ambapo takribani vijana 1,200,000 humaliza elimu ya vyuo mbalimbali kila mwaka na kati yao ni vijana 200,000 huajiriwa kwa mwaka. 

Pia Ikumbukwe kuwa Vijana wanachukua asilimi 68 ya nguvu kazi ya Taifa lakini takwimu zinaonyesha kuwa upungufu wa ajira kwa Vijana ni asilimia 14.4.

Hivyo serikali imetoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo ambayo  haimuhitaji mkopaji kuwa na dhamana isiyo hamishika bali kuwa na uaminifu wa kurejesha mkopo huo utakaotolewa kupitia vyama vya kuweka na kukopa SACCOS.

Hivyo Vijana mnashauriwa kujiunga katika vikundi na kufanya mawasiliano na Maafisa Vijana katika Halmashauri zenu ili kujua taratibu za kupata mikopo hiyo.

Zingatio kwa mkopo huu
Walengwa
Vijana wenye umri kati ya miaka 15-35
Riba
Asilimia kumi kwa mwaka (10%)
Mikopo itatolewa kupitia Saccos za Vijana. 

Cha msingi ni kujiunga katika vikundi, kujisajili, kutengeneza mchanganuo wa biashara na mwishowe mnakwenda halmashauri kuomba mikopo hiyo, pale halmashauri utakutana na maafisa maendeleo wa kata mitaa na wilaya ambapo watakupa utaratibu kamili ili upate mkopo huo, cha msingi wewe jitambulishe tu kwamba umekwenda pale kwa ajili ya MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA
Pia tembelea: http://apf-tanzania.ning.com/profiles/blogs/youth-development-fund-ydf-targets-youth-in-groups

0 comments:

Post a Comment