Saturday, June 8, 2013
On 4:32 AM by Shambani Solutions No comments
![]() |
Tumetoka Mbali; Mwenyekiti Wenu Kwenye Shamba Lake La Viazi 1991! |
Pichani ni kijijini Igagala, 1991. Ndio kwanza nimetoka
kwenye Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT)- Operesheni Kambarage. Na nimekondeana
pia, lakini , ni mwenye nguvu za kulima!
Naam, kwa hiyari yangu, na kwa vile sikupata kuishi
maisha ya kijijini kwa muda mrefu, nikaamua kuishi maisha ya kijijini kwa mwaka
mmoja na nusu. Niliishi kijijini Igagala wilayani Njombe, mbali kabisa na Dar
es Salaam nilikozaliwa na kukulia. Nilitaka kuishi na kujifunza maisha ya
kijijini. Ndio, nilitaka kuyafahamu kwa karibu maisha ya wanavijiji wa nchi
hii. Kuwaelewa wanavijiji wanavyofikiri.
Hivyo, miongoni mwao nami nilikuwa mkulima kijana
wa zao la viazi. Wakati huo, mbolea ya kupandia aina ya ’ DAP’ tulinunua kwa
shilingi elfu tano kwa mfuko mmoja wa kilo 50. Ulitosha ekari moja. Bei ya sasa
ni zaidi ya shilingi themanini elfu. Mbolea ya Urea na ’ CAN’ enzi hizo
tulinunua kwa shilingi elfu nne. Sasa inauzwa kwa zaidi ya shilingi sabini
elfu. Gharama zote hizo bado hujaongeza gharama za kuifikisha mbolea shambani.
Naam, tumetoka mbali.
Picha kwa hisani ya Mjengwablog,
Iringa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment