Friday, March 29, 2013

On 9:54 AM by Shambani Solutions   No comments



Safari hii hajaja  sokoni kuchukua fedha kwa njia haramu au ya vitisho, lakini kulipwa kwa magunia matatu ya spinachi na sukuma wiki aliyoyaleta alfajiri, ikiwa ni sehemu ya maisha yake mapya tofauti na makosa ya vurugu.

Irungu alikuwa ni mmoja kati ya majambazi walioogopwa sana katika viunga vya Mathare, Huruma na Eastleigh huko Nairobi, lakini sasa anaishi maisha ya kawaida kwa kujipati riziki yeye mwenyewe pamoja na familia yake kwa kilimo cha mjini.

Kwa hiari yake na majirani zake, Irungu alikuwa akivunja nyumba na kuvamia na kufanya vitendo vingine vya vurugu za uhalifu hadi Oktoba 2010. Wakati huo, polisi waliingilia kati kundi lilipojaribu kumpiga Irungu na majambazi wengine kwa wizi wa pikipiki kutoka mbele ya duka la bidhaa mbalimabali. Irungu alinusurika katika kundi hilo, lakini alifungwa jela kwa mwaka mmoja.

Baada ya miezi kadhaa, wakati wa kukutana kwa majambazi katika eneo la ujenzi, jambazi mmojawapo alipendekeza kwamba badala ya uhalifu, wanaweza kulima ardhi ya serikali isiyolimwa katika viunga vyao. "Tulichangishana fedha sisi wenyewe na baadhi ya majirani walikuja na msaada wa vifaa na fedha," Irungu aliiambia Sabahi.

Kutoka katika uhalifu hadi kuzalisha mbogamboga
Mwaka jana, Irungu na majambazi wenzie wa zamani walianzisha Kikundi cha Vijana Wakulima wa Mathare, kikundi kimojawapo kati ya vikundi kadhaa visivyokuwa rasmi ambacho kinazalisha matunda na mbogamboga katika makazi duni. "Kwa mwezi, shamba linaweza kunipatia zaidi ya shilingi 50,000 (Dola 590) baada ya kutoa gharama za uzalishaji," alisema Irungu.

Muiruri Wangethi, mwenye umri wa miaka 20, jambazi mwingine wa zamani aliyebadilika na kuwa mkulima, pia alihukumiwa mwaka mmoja jela kwa kuiba pikipiki mwaka 2011, lakini kupitia mpango wa serikali wa kupunguza msongamano katika magereza, aliwekwa katika uangalizi baada ya kukaa jela miezi miwili.  "Sasa tuna uwezo wa kuzihudumia familia zetu kwa njia halali," aliiambia Sabahi. "Tunajutia sana muda wetu tulioutumia kwa shughuli za uhalifu na tutaendelea kujaribu kwa uwezo wetu kufidia muda tulioupoteza."

Wahalifu waliobadilishwa kutoka katika ujambazi wamefuata njia ileile kwa kuunda umoja wa kilimo pembezoni mito na vijito katika mji mkuu wa Kenya, alisema. Vikundi vya ushirika vinalima matunda ya mapesheni, pilipili, miwa, vitunguu, nyanya, mahindi, maharage, magimbi, viazi vitamu na mviringo, mihogo, koliflawa na mboga za majani ambavyo wanaviuza katika masoko yalioko Nairobi. 

Antony Macharia, mwenye umri wa miaka 33, mhalifu aliyejirekebisha aliyejiunga katika kilimo cha ushirika kupitia uanachama wa Kikundi cha Wakulima wa Mathare Ghetto, alisema vijana waliojirekebisha pia wanasaidia polisi jamii."Taarifa zetu za nyuma zisizofutika zinatufanya washukiwa wa kwanza kila uhalifu unapofanywa katika maeneo ya jirani," aliiambia Sabahi. "Tumeamua sisi wenyewe kuhakikisha uhalifu unapungua."
Kikundi chake chenye watu nane mara kwa mara hufanya mikutano katika ukumbi wa mji kuwatahadharisha vijana dhidi ya kufuata nyayo zao za uhalifu. Pia wanafanya kazi na jamii na kuwahamasisha wale wanaojihusisha na uhalifu kuachana na mtindo huo haramu wa maisha, alisema. 

Kuiweka ardhi katika matumizi mazuri

Mkuu wa Wilaya ya Mathare Gerald Omoke amekadiria kwamba waliokuwa wahalifu 200 sasa wamekuwa wakulima kando ya mto badala ya kujihusisha katika uhalifu. 
Ardhi ambayo vijana wanalima ilikuwa imetengwa kwa matumizi mengine, lakini serikali inaruhusu kwa muda matumizi hayo ya kilimo ili kuwasaidia waliokuwa wafungwa kuishi maisha ya uzalishaji na ya uhakika, alisema."Ili kukomesha uhalifu na shughuli za uhalifu, tunawahamasisha watu kujihusisha katika miradi yoyote [halali] inayozalisha kipato, na kilimo ni kimoja wapo," aliiambia Sabahi.Mtindo huo unasambaa maeneo ya jirani ya Kayole, Njiru, Ruai, Mihang'o, Dandora na Korogocho, 

alisema. Baada ya maombi ya vyama vya ushirika mbalimbali, mara kwa mara maofisa kilimo wa serikali hutembelea mashamba kuwafundisha wakulima vijana stadi na mbinu za kuongeza mavuno ya mazao, Omoke alisema. 

Jecinta Awino, mwenye umri wa miaka 42 na muuza duka la vyakula na bidhaa huko Mathare, alisema inachukua muda mrefu, lakini sasa wakaazi wenyeji wanatambua kwamba waliokuwa wanachama wa kundi wamejirekebisha wenyewe. "Kuna mahitaji ya chakula na kama mtu akipata mazao freshi moja kwa moja kutoka jirani bei inakuwa rahisi kwa sababu hakuna gharama za usafiri zinazohusishwa," alisema. Peter Ongori, mwenye umri wa miaka 35, mkazi wa mtaa wa Kayole, alisema huduma zaozinathibitisha kufaa sana. "Bado wanahitajika sana, sio kwa uhalifu wao wa siku za nyuma, bali kwa mazao yao freshi," alisema.

0 comments:

Post a Comment